Definition List

.
Latest Post

FALSAFA YA MAISHA YA MUISLAMU II

Written By binally on Sunday, April 20, 2014 | 10:55 PM



NINATOKA WAPI?
                                                                              

Hili ni swali la pili la msingi. Watu wengi wamejaribu kutafuta jibu la swali hili, hata wengine wakabuni kuwa binadamu ametoka ghafla kwa bahati  nasibu. Mwaka 1971 Sharman M, mwandishi wa kitabu cha “Man, Civilization and Conquest” anasema “in the beginning 5000 million years ago, the Earth was spinning in space millions of years before there were any living plants or animals on it. 200 million years ago, there were plants, animals and birds on Earth millions of years before man appeared…..in 2 million years ago, there were also apes. Some of the apes after countless generations and more million years, became man-like….their brains become larger and their intelligent grew(uk 1) hii yaonesha kuwa hakukuwa na dalili ya uumbaji kwa fikra zao ila ni mabadiliko tu ya kimaumbile ambayo yalikuwa yakitokea baada ya miaka milioni kadhaa na tena baada ya milioni kadhaa tena mabdiliko mengine yanatokea hata kuja kupatikana kwa sokwe ambaye naye baada ya miaka milioni kadhaa akawa binadamu kamili.Hii ni sababu ambayo kimsingi haina msingi wa kiakili, kwa sababu ikiwa hata utando wa buibui hauwezi kutokea kwa bahati nasibu, iweje binadamu na mpango wake wa kimaumbile atokee kwa bahati nasibu?. Wengine wanasema kuwa mtu alianza kuwa nyani ndipo akabadilika taratibu hadi akawa mtu huyo ni Charles Darwin katika kitabu chake “The Origin Of Species”, na Sharman 1971, anasema “the gorillas and chimpanzees are put into our family tree because they are (our) remote COUSINS” yaani sokwe na nyani hawa ni ndugu zetu wa mbali.
                                                                             

Huu ni uongo ambao hadi leo unafundishwa mashuleni. Hata hivyo hadi leo manyani ni manyani na watu ni watu tu na hakuna kiumbe yeyote aliyewahi kuonekana sehemu yeyote duniani akiwa nusu mtu nusu nyani akiwa bado yupo katika hayo mabadiliko. Sisi waislamu tunasema hakuna binadamu atayeweza kutuambia sisi binadamu asili yetu nini au tunatoka wapi kinyume na anavyotueleza Yule alotuumba. Watu wote sisi  ni wageni katika hii dunia hivyo hivyo ni muhali kutokea mtu akajifanya mwenyeji sana kiasi cha kujua asili ya watu wakati yeye naye kajikuta katika duniani kama binadamu wengine. Hivyo mwenyezi mungu pekee ndio anayeweza kutuambia sisi tunatoka wapi na asili yetu ni nini, Allah anasema
 76:1
            “hakika ulimpitia binadamu katika dahali hakuwa ni mwenye kutajwa”(76:1) 
 Aya hii inatuambia kuwa kuna wakati tena mrefu tu ambapo mwanadamu hakuwapo kabisa, hivyo ni wazi kuwa alikuwa na mwanzo. Kuhusu mwanzo huu Allah anatuambia
 15:28
na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika hakika MIMI nitamuumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti,wenye kutokana na matope yaliyovunda!(15:28) 

Aya hii inatupasha habari ya kuumbwa kwa mtu baada ya muda mrefu kupita bila ya kuwepo dunia.Mtu aliumbwa kwa udongo, pengine mtu anaweza kubishia maelezo haya ya kuwa kaumbwa kwa udongo, maana inaweza kuwa vigumu kwake kulinganisha mwili wake unaowaka kwa mafuta na udongo. Lakini  kwa vile huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia, tunaweza kuhakikisha maneno ya mwenyezi mungu ni ya kweli pasi na shaka kwa kuangalia uhusiano wa udongo na mwili wa binadamu. Ukichunguza mwili wa binadamu utakuta una aina mbalimbali za madini kama vile chuma,calcium,phosphate,iodine n.k ambayo mtu hawezi kuyapata sehemu yeyote ila ARDHINI kwenye udongo,hivyo basi kuna uhusiano mkubwa kati ya mwili wa mtu na udongo .vilevile ukichunguza mahitaji ya mwili wa binadamu anahitaji vitu hivi kwa mahitaji ya mwili wake na vitu hivi vipo ardhini lakini kwa udhaifu wake hawezi kuvipata, Allah (sw) kwa rehma zake akamuumbia mimea na kisha ile mimea akaipa kazi, kwa kila mmoja kufyonza aina fulani pekee ya madini. Kwa mfano, muwa unafyonza sukari kutoka ardhini na kuhifadhi katika shina lake ili mtu aipate kiurahisi, wanga unafyonzwa kupitia ngano,mahindi,mpunga n.k, mafuta yanafyonzwa na ufuta,alizeti,karanga,minazi,pamba n.k na protini inafyonzwa na mimea yenye asili ya maharagwe kama vile kunde,mbaazi,maharagwe n.k vyote hivi vinafyonzwa kutoka ardhini/udongoni ili vitumike kujenga mwili uloumbwa kwa udongo hivyo ni lazima ujengwe kwa asili yake ambayo ni UDONGO
                                                                


Mwenyezi Mungu anatukumbusha kwa kusema
80:2480:25
 80:26

Hebu mtu na atazame chakula chake.Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu.Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu. Kisha tukaotesha humo nafaka,Na zabibu, na mimea ya majani,Na mizaituni, na mitende, Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,Na matunda, na malisho ya wanyama; Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. (80:25-32)

Chakula ndicho kina mahitaji ya mwili hivyo Allah katika aya hii anatupa picha jinsi ya vyakula aina mbalimbali vinavyotokana na mimea ya aina mbalimbali inayoota baada ya kupasuliwa ardhi kuonesha jinsi gani mwili wa binadmu ulivyo na mahusiano na ardhi/udongo. Na katika kusisitiza hilo Allah anasema (55:14)

55:14
                                                       Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo
 Picha anayotupa Allah (SW) hapa ni kuwa mtu aliumbwa kama sanamu iliyofinyangwa(fakhaari)
Na kumbuka 15:28-29) "Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia."

Hapa tunapata habari kwamba baada ya Allah kumuumba mtu kwa udongo kama sanamu, akampulizia roho, akampa uhai, na ndipo mtu akawa mtu kama tunavyomfahamu, anaona, anasema, anasikia n.k

Hivyo tunamalizia jibu letu la asili ya mwanadamu kwa kusema Binadamu ana Asili mbili:
ü                Asili ya UDONGO, ambao ni asili ya kitu duni na
ü                Asili ya ROHO, ambayo ni asili ya kitu kitukufu sana.
                                                                                               itaendelea................

JE wajua WE MWANAMKE


Kuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala amekuamrisha kuvaa Hijabu?
Mwenyezi Mungu anasema;
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiisalamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.”
Al Ahzab = 59

Je! Mnazijuwa sifa za hijabu walokuwa wakivaa Masahaba wanawake (RA)?
Anasema Aisha (RA);
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alikuwa akeshamaliza kusalisha sala ya asubuhi (Alfajiri) wanawake huondoka wakiwa wamejifunika vitambaa vyao hawajulikani kutokana na giza wala hawatambuani wenyewe kwa wenyewe.”
Bukhari na Muslim

Je unajuwa kuwa kuonyesha mapambo ni katika matendo ya wakati wa ujahilia?
Mwenyezi Mungu anasema;
“Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili (zama za ujinga – ukafiri).”
Al Ahzab – 33

Je unajuwa kuwa kujifananisha na makafiri kwa mavazi kunakufanya uwe mfano wao?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Atakayejifananisha na kaumu yuko pamoja nao.”
Ahmed na Abu Daud – na hadithi hii ni njema.

Je unajuwa kuwa Pepo imeharamishwa kwa wenye kuonyesha mapambo yao?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Aina mbili ni watu wa motoni sijapata kuwaona: Wanawake waliovaa huku wakenda uchi, wanayumba wakiyumbisha, vichwa vyao mfano wa nundu la ngamia lililoelemea upande mmoja. Hawatoingia Peponi wala hawataionja harufu yake.”
Muslim

Je unajuwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amewalani wanawake wanaojifananisha na wanaume?
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amewalani wanaume wanaovaa nguo za kike na wanawake wanaovaa nguo za kiume.”
Abu Daud na Ibni Majah na hadithi hii ni sahihi.

Je unajuwa kuwa haijuzu kuvaa nguo nyepesi?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alisema kumwambia Osama bin Zeid;
“Mbona hujakivaa kile kitambaa kilichotoka Misri?”
Akasema;
“Nimempa mke wangu.”
Mtume (SAW) akamwambia;
“Mwambie  avae shumizi chini yake  kwani naogopa isije ikabainisha umbile lake.”
Ahmed na Al Baihaqiy na hii ni hadithi njema

Je unajuwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) ameamrisha kuacha kujipamba na kujipaka mafuta mazuri wakati wa kutoka?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Msiwazuwie wanawake kwenda misikitini, (lakini) watoke bila kujipaka mafuta mazuri.”
Muslim

Je mnajuwa kuwa kujipaka mafuta mazuri mbele ya wanaume ni sawa na kuzini?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
“Mwanamke yeyote atakayejipaka mafuta mazuri kisha akapita mbele ya kundi wakaisikia harufu yake anakuwa keshafanya kitendo cha zina.”
Abu Daud – Attirmidhiy – Annasai na hadithi hii ni sahihi

Je unajuwa kuwa mwanamke wa kiislamu hapigani vikumbo na wanaume?
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) alitoka msikiti akaona mchanganyiko wa wanawaume na wanawake njiani.
Mtume (SAW) akasema;
“Jichelewesheni kwani haipasi kwenu kupita kati kati ya njia, piteni kando ya njia.”
Wanawake wakawa wanakwenda wakijibana na ukuta hata nguo zao zilikuwa zikiganda ukutani kutokana na kujibana kwao.
Abu Daud – hadithi njema

ZIJUE NYOYO



Nyoyo zina njia zake sita. Tatu katika hizo ni ovu, na tatu nyengine ni njema.

Zilizo ovu, siku zote;
  • Zinapambiwa na dunia, au
  • Zinaidanganya nafsi yake na Kuadhibika katika dunia, au
  • Huwa zina adui anayezijaza wasi wasi na kuisababishia adhabu hiyo.
Ama njia tatu njema, ni zile
  • Zinazotenda mema na kuonekana natija yake, au
  • Zenye kuwa na akili inazoziongoza, na
  • Zenye kumjua Mola wake ili zimuabudu kama anavyopaswa kuabudiwa.
Nyoyo zote zinatembea katika njia hizi.sita.
Kufuata matamanio ya nafsi, na kuwa na matumaini ya kuishi muda mrefu, ni
katika sababu kubwa ya kufisidika kwa moyo, na kufuata matamanio ya
nafsi kunasababisha kuupofosha moyo huo usiweze kuuona ukweli na usiweze kuiona haki.
Kufuata matamanio ya nafsi kunamfanya mtu asipate raha, na siku zote hupenda
kujishambulia au kushambulia wenzake.
Kuwa na tamaa ya kuishi mda mrefu hapa duniani, kunamfanya mtu aisahau
akhera yake na kumzuwia asijitayarishe nayo..

Mwenyezi Mungu anapomtakia mja wake kheri, humjaalia kuwa ni mtu
anayekubali kuwa yeye ni mtenda madhambi na kujizuwia kufuatilia madhambi ya
wenzake.
Humjaalia pia asipende kuwanyima wenzake kile alicho nacho katika mambo ya kheri, na kutopenda kufuatilia vya wenzake.
Na iwapo Mwenyezi Mungu hamtakii mja wake kheri, basi huyageuza mambo, na kuyafanya yawe kinyume na hivyo.
Mtu anapoiona kheri katika nafsi yake, basi amshukuru Mwenyezi Mungu.
Ama anapoona kinyume cha hivyo, basi ailaumu nafsi yake.

Kwa hivyo mtu anatakiwa ajaribu kuzijuwa zile sifa njema ili aweze kuzifuata na kuzipenda.
Na pia anatakiwa atambuwe neema alizopewa na Mola wake ili aweze kumshukuru
kwa kuongeza utiifu.

SIFA ZA NAFSI YA HALI YA JUU
Shaqiyq Ibrahim Al Balkhiy, mmoja katika wanavyuoni wakubwa aliyefariki katika mwaka wa 194H. alisema;
"Watu wa aina sita hufungiwa milango ya kufanikiwa;
Wanaojishughulisha na neema wakasahau kumshukuru aliowaneemesha.
Wenye kujishughulisha kutafuta elimu kisha wasiifanyie kazi.
Wepesi wa kufanya madhambi na wazito wa kutubia.
Wanaopenda kufuatana na watu wema wakaacha kufuata mwenendo wao.
Wanaoikimbilia dunia na hali dunia inawakimbia, na
Wanaoikimbia akhera wakati akhera inawakimbilia wao".

Ama Ibnil Qayim, yeye anasema;
"Yote hayo yanatokana na kutokuwa na uoga - uoga wa kumuogopa Mwenyezi Mungu - na asili yake hasa ni upungufu wa yakini na upungufu wa ilimu - ilimu ya kumjua mtu Mola wake, na asili yake hasa ni mtu kuwa na nafsi dhalili na nafsi duni inayokubali kubadilisha kile kilichokuwa duni kwa kile kilichokuwa bora, ama sivyo kama nafsi ingekuwa tukufu inayojiheshimu, basi isingeridhika na kilichokuwa duni".

Heshima Ya Nafsi
Anaendela kusema Ibnil Qayim;
"Kwa hivyo asili ya kheri yote imo katika kuiheshimu mtu nafsi yake hiyo na katika kuitukuza kwake na katika kuitakasa kwake. Na asili ya shari yote imo katika kuidharau mtu nafsi yake na katika kuiviza na katika kutoiheshimu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Bila shaka amefaulu aliyeitakasa (nafsi yake) Na bila shaka amejikhasiri aliyeiviza (nafsi yake)".
Suratush shams - 9-10
Na maana yake aya hii ni kuwa; 'Imefuzu nafsi ya yule aliyeilea katika kumcha Mungu na katika kuitakasa na katika kuikuza kwa kumtii Mwenyezi Mungu. Na imekula hasara nafsi ya yule aliyeilea katika kumuasi Mwenyezi Mungu na katika kuichafua na kuidogosha.
Kwa hivyo nafsi zinazojiheshimu haziridhiki isipokuwa kwa yaliyo matukufu na yaliyo bora na yenye mwisho mwema. Na nafsi zilizo duni ziku zote zinayazungukia zungukia yaliyo duni na kuyaangukia kama nzi wanavyoangukia uchafu.
Kwa ajili hiyo nafsi zinazojiheshimu haziridhiki na dhulma wala haziridhiki na uchafu wala wizi wala khiyana. Na hii ni kwa sababu nafsi hizo ziko juu na zimetakasika mbali kabisa na mambo kama hayo.
Ama nafsi dhalili zisizojiheshimu zinakwenda kinyume kabisa na hayo, kwani kila nafsi inaelekea kule inakopendezwa nako.
Na hii ndiyo tafsiri ya kauli yake Subhanahu wa Taala aliposema;
"Sema; "Kila mmoja anafanya (amali yake) kwa njia yake."
Bani Israil -84
Yaani anafanya kazi kwa njia ile anayonasibiana nayo, kwani anafanya kufuatana na vile anavyopenda na kunasibiana na mwenendo na tabia zake. Na kila nafsi inakwenda katika njia yake na mwenendo wake inaoupenda na kuuelekea.
Kwa hivyo mtu asi anafanya amali zile zinazonasibiana na mwenendo wake katika kuzilipa neema alizoneemeshwa nazo kwa uasi na kwa kwenda kinyume na yule Aliyemneemesha. Na Muislam aliyeamini kikweli anafanya amali zake zinazonasibiana na mwenendo wake katika kumshukuru na kumpenda yule Aliyemneemesha, na pia katika kumsifia na kumtukuza na kumuadhimisha na kujipendekeza kwake na kumuonea haya pamoja na kuchunga asimuasi. "

 na MUHAMMAD FARAJ SALEM AL SAIY

Dua zilizomo katika Qur'ani

Written By binally on Saturday, April 19, 2014 | 3:52 PM



رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ [٢:١٢٧]
Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi [al-Baqarah 2:127]
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ [٢:١٢٨]
Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [al-Baqarah 2:128]
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ [٢:٢٠١]
Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! [al-Baqarah 2:201]
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٢:٢٥٠]
Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri [al-Baqarah 2:250]
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٢:٢٨٦]
Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri [al-Baqarah 2:286]
رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ [٣:٨]
Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji [Aal ‘Imraan 3:8]
رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ [٣:٣٨]
Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi. [Aal ‘Imraan 3:38]
رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٣:١٤٧]
Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. [Aal ‘Imraan 3:147]
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ [٧:٢٣]
Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. [al-A’raaf 7:23]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ [٧:٤٧]
Mola Mlezi wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na madhalimu (watu walio dhulumu.) [al-A’raaf 7:47]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ [١٠:٨٥]
Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. [Yoonus 10:85]
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [١٠:٨٦]
Na utuokoe kwa rehema yako kutokana watu makafiri. [Yoonus 10:86]
رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا [١٨:١٠]
Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu. [al-Kahf 18:10]
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ [١٤:٤٠]
Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. [Ibraaheem 14:40]
قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي [٢٠:٢٥]
وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي [٢٠:٢٦]
وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي [٢٠:٢٧]
Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu 
[Ta-Ha 20:25-27]
رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا [٢٠:١١٤]
Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu [Ta-Ha 20:114]
لَّا إِلَٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ [٢١:٨٧]
Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. [al-Anbiya’ 21:87]
رَّبِّ أَنزِلْنِي مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ الْمُنزِلِينَ [٢٣:٢٩]
Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji. [al-Mu’minoon 23:29]
رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ [٢٣:٩٧]
Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. [al-Mu’minoon 23:97]
وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ [٢٣:٩٨]
Mola wangu Mlezi, wasinikaribie. [al-Mu’minoon 23:98]
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ [٢٦:٨٣]
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. [al-Shu’ara’ 26:83]
رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ [٢٨:٢١]
Mola wangu Mlezi! Niokoe na watu madhaalimu. [al-Qasas 28:21]
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا [٢٥:٧٤]
Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu. [al-Furqaan 25:74]
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ [٢٧:١٩]
Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema. [al-Naml 27:19]
رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا [٢٥:٦٥]
Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi. [al-Furqaan 25:65]

FALSAFA YA MAISHA YA MUISLAMU I

Written By binally on Tuesday, April 15, 2014 | 2:26 PM




MAISHA YA MUISLAM
Mwanadamu katika maisha yake yote hana budi kufahamu ana jukumu gani akiwa kama mwislamu katika dunia hii. Suala hili linakuja pale mwislamu anapojitambua (self-actualization) na kujitambua hakuwezekani mpaka mwislamu huyu ameweza kujibu maswali haya:-
*      Mimi ni nani?
*      Ninatoka wapi?
*      Niko wapi na kwanini?
*      Ninaelekea wapi?
*      Mwisho wangu utakuwa nini?

Haya ni ndio tunayoyaita maswali ya msingi. Mwislamu anapoweza kujibu maswali haya na akazingatia majibu yake tunasema mtu huyo amejitambua iliyobaki ni kutekeleza tu katika utendaji wa kitu chochote kujitambua ndio jambo la msingi la kwanza kabisa. Kwa mfano: Meneja hawezi kuwa meneja mzuri kama hajitambui kwa maana kwamba haelewi ilikuwa meneja mzuri anatakiwa awe vipi na afanye mambo gani yanayomwajibikia, vivvyo hivyo muislamu hawezi kuwa muislamu safi kama haelewi aweje na aishi vipi.
Katika Makala hii tutajaribu kutoa maelekezo ya majibu fasah ya maswali haya ya msingi yanayomuwezesha muislam ajitambue na aishi kweli kama muislamu.

MIMI NI NANI?

 

Mtu anapoulizwa wewe ni nani mara nyingi hukimbilia kutaja jina lake. Kwa mfano: akasem mi ni kibabu, juma,zawadi,zainabu au kandoro. Lakini ukweli ni kuwa yeye si kibabu, si juma, si zawadi au kandoro kwani hili ni jina tu, kama ilivyo kwamba anashati,suruali, gauni na viatu.Sasa gauni, shati, suruali na viatu ambavyo vyote ni vyake tukiviweka pembeni yeye anabaki kuwa ni NANI? Kwa sababu kama ambavyo anaweza kubadilisha shati lake ,gauni au suruali na vitu vingine na jina pia anaweza kubadilisha. Yeye ni kile kisichoweza kubadilika. Vilevile anaweza kujibu mimi ni MTU. Bado jibu hili sio sahihi sana kwa vile hata UTU anaweza asiwe nao pia akawa na tabia za kinyamatu.Hivyo utu pia hubadilika hivyo mtu atatoa jibu fasaha na sahihi lisilo na utata kama atajibu mimi ni KIUMBE. Mtu anapojitabulisha kwamba ni kiumbe ni wazi kuwa anatambua asili ya kiumbe chochote kile ni kuumbwa na kukubali kwake kuwa kiumbe ni wazi kuwa anakubali yeye kaumbwa. Na ili ajitambue vyema ni lazima afahamu kaumbwa na nani. Hii ni wazi kwani hata mtoto mdogo hutambua kuwa amezaliwa na anapojitambulisha vizuri humtaja baba yake. Kiumbe anayejitambulisha vyema humjua muumba wake, SISI waislamu tunatambua muumba wetu ni MWENYEZI MUNGU (SW) hata watu wengine ambao sio waislamu wanatambua kuwa yupo muumba ingawa wanapuuzia ukweli huu au kumshirikisha.

NINATOKA WAPI?
itaendelea..........

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Mubaarak Youth Islamic Community - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger